
Kufanya maamuzi ni jambo endelevu kwa kila mfanya biashara, baadhi ya maamuzi hayo yanaweza kuhusisha mabadiliko ya bei ya bidhaa ama huduma, kujengea jengo jipya katika kupanua biashara, mkuajiri wafanyakazi wa ziada, upanuzi wa masoko, matumizi fedha na kadhalika.
Maaamuzi huweza kuleta madhara ama faida katika biashara. Basi haina budi maamuzi yote ya kibiashara kwa uangalifu mkubwa. Endapo maamuzi haya yatafanywa bila kuzingatia mambo muhimu hupelekea madhara katika biashara na endepo yatafanywa katika kuzingatia mambo muhimu basi hupelekea mabadiliko mazuri ama faida katika biashara.
Je maamuzi sahihi ya kibiashara ni yapi? Ni maaamuzi ambayo yamefanyika kwa kuzingatia vigezo vyote vilivyopo katika kuchambua uhusiano na uwiano wa vigezo husika ili kufikia maamnuzi ambayo hutoa fulsa za maendeleo kibiashara kulingana na malengo, maono na mikakati ya biashara husika. Kama vile kiwandani huwezi tegemea kupata bidhaa bora kama hutahusisha malighafi bora na utaratibu mzuri katika utegenezaji wa bidhaa husika.
Kwa mfano maamuzi ya kupandisha ama kushusha bei ya bidhaa au huduma, muhusika lazima azingatie mambo muhimu;-Sababu za mabadiliko ya bei ya bidhaa, muda wa mabadiliko, tofauti ya bei kati ya mfanya biashara mmoja na mwingine, matarajio baada ya mabadiliko, faida katika mauzo, jinsi sahihi ya kuelimisha wateja kuhusu mabadiliko ya bei n.k.
Ukweli ni kwamba ubora wa maamuzi hujulikana kutokana na ubora wa matokeo ya maamuzi. Matokeo ya maamuzi mengi tuyafanyayo hutokea muda ujao na muda ujao hautabiriki, basi jambo la muhimu ni kuzingatia njia zitumikazo katika kuchanganua vigezo vyote ili kufikia maamuzi sahihi, ambapo katika mchanganuo huo ni kujitahidi kuondoa vigezo vyote ambavyo vinaweza kusababisha kutofanikiwa kwa maamuzi bora.
Kwa hiyo, ni muhimu mhusika kupata muda wa kutosha kutafuta vigezo vyote ama taarifa za kutosha katika kufikia maamuzi na kuangalia mahusiano an uwiano na matarajio au matokeo ya kila kigezo endapo kitahusishwa katika kufanya maamuzi. Endapo kigezo kimoja kitakosekana kwa sababu moja ama nyingine basi thamani ya maamuzi hayo hushuka. Kwa hiyo ni vema kabisa kuhusisha vigezo au taarifa nyingi iwezekanavyo katika kufikia maamuzi.
Kazi ya kutafuta vigezo sio rahisi kwani huusisha kufikiri sana na penginepo huilazimu kuhusisha wadau wengine ili nao waweze kutoa mchango wao. Katika makampuni makubwai huwepo bodi ya wakurugenzi ambao hutumika kama washauri wakuu wa biashara ama kampuni, tofauti na kwenye biashara ndogo ndogo mara njingi mengi kufanywa na mtu binafsi, mhusika mkuu wa biashara. Basi ni muhimu kwa wenye biashara ndogo ndogo kujifanyia mahusiano mazuri wa wafanyabiashrara wengine wenye uzoefu , kuhudhuria semina za mafunzona kujiunga kwenye taasisi za kibiashara ili ufikapo muda wa kufanya maaamuzi muhimu ya kibiashara waweze kupata ushauri na ufahamu wa kutosha ili kukabiliana na suala husika.
Baada ya kufanya maamuzi , ni muhimu kuweka muda wa utekelezaji wa maamuzi , dunia ya sasa hubadilika kila kukicha na endapo utekelezaji wa maamuzi hayatafanyiwa kazi katika muda muafaka basi jambo husika linaweza kupitwa na wakati. Kwa hiyo basipo utekelezaji wa maamuzi kwa muda muafaka itakuwa hakuna umuhimu kujitahabisha wa kufanya maamuzi yoyote. Mara nyingi maamuzi mengi yaliyo sahihi hufanyika lakini hufia mbali kwa kukosa utekelezaji.
Wafanya maaamuzi sio lazima wawe watekelezaji , hapa suala la mawasiliano huchukua umuhimu ambapo wafanya maamuzi hutakiwa kufikisha ujumbe sahihi kwa watekelezaji. Ni vema kuwa na utaratibu mzuri wa kuwafahamisha watekelezaji umuhimu wa maamuzi hayo na matarajio ama mategemeo yake hapo baadaye. Kwa kufanya hivyo , kunakua na muunganiko dhabiti na msukumo wa kutosha katika kufanikisha maaamuzi husika.
No comments:
Post a Comment